Friday, July 1, 2011

Simba yajihakikishia kucheza robo fainali Kagame Cup

Timu ya Simba ya Tanzania leo hii imejihakikishia kucheza hatua ya Robo fainali baada ya kuifunga Etincelles ya Rwanda kwa jumla ya magoli 2-0 katika mchezo wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam Tanzania.

Magoli ya Simba yamefungwa na Haruna Moshi katika kipindi cha kwanza na Mussa Hassan Mgosi kipindi cha pili.

Katika mechi ya awali ya kundi hilo la A Red Sea ya Eritrea imebamiza Vital'o ya Burundi kwa goli 1- 0

No comments: