Saturday, October 20, 2012

BREAKING NEWS!!!!!: Sheikh Farid wa Uamsho anayedaiwa kutekwa amepatikana

Sheikh Farid Hadi Ahmed kiongozi wa kundi la Uamsho Zanzibar
Habari ambazo tumezipata hivi punde kutoka Zanzibar zinasema Sheikh Farid Hadi Ahmed kiongozi wa kundi la Uamsho aliyedaiwa kutekwa sasa ameonekana na hivi yupo nyumbani kwake Zanzabar.

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinasema Sheikh yupo na ni mzima japo hakuna taarifa zaidi kwamba alikuwa wapi kwa siku tatu mfululizo..

Kupotea kwa Sheikh Farid kumesababisha vurugu kubwa huko visiwani Zanzibar kutoka kwa wafuasi wa kundi la Uamsho ambao walichoma makanisa na ofisi za Chama cha Mapinduzi ikiwa ni pamoja na kutishia kuwadhuru viongozi wa dini ya Kikristo.

Tutaendelea kuwaletea zaidi taarifa kwa kadri tutakavyokuwa tunazipata.

No comments: