Monday, October 15, 2012

CCM Bwana!!! wee acha tu!! Makongoro naye chali

Makongoro Nyerere
 MWENYEKITI wa CCM, Mkoa wa Mara aliyekuwa akitetea nafasi yake, Makongoro Nyerere, ameshindwa kutetea kiti hicho. Makongoro ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ameshindwa kutetea kiti chake, baada ya kushindwa katika uchaguzi uliofanyika jana katika Shule ya Sekondari Songe linaripoti gazeti la Mtanzania.

Kutokana na hali hiyo, aliyeshinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mara ni Christopher Sanya.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Nazir Karamagi, alisema Sanya ndiye Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Mara baada ya kupata kura 481.

Alisema Makongoro alipata kura 422 na mgombea wa tatu aliyewahi kushika nafasi hiyo mwaka 2005 ni Enock Chambiri, aliyepata kura 140 wakati kura tisa ziliharibika.

Kabla ya matokeo kutangazwa rasmi, Sanya alikuwa amepata kura 469, Makongoro Nyerere, kura 402 na Enock Chambiri kura 144 kati ya kura 1012 zilizopigwa ambapo kura 1 iliharibika.

Pamoja na uwepo wa matokeo hayo, kura zilipigwa tena baada ya kuonekana mshindi kupata kura ambazo hazikuvuka nusu.

Pamoja na kukubali matokeo, Makongoro alitoa nasaha kwa Sanya na kumshauri kuwa muadilifu na kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

“Kazi ya uenyekiti si lelemama na mkoa huu ni mgumu sana kuuongoza, wewe ndiye kiongozi mkuu wa mkoa huu, katika kupanga mikakati ya kushinda uchaguzi mwaka 2015.

Kwa upande wake Sanya aliwashukuru wajumbe waliompigia kura na kuahidi kuyafanyia kazi, yote aliyoelezwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake.

Katika nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, walipatikana washindi wawili wawili kila wilaya.

Walioshinda kutoka Wilaya ya Serengeti ni Josephat Seronga na Ester Nyarobi, wakati Zuhura Makongoro na Jackson Waryoba, walishinda kupitia Wilaya ya Bunda na Josehat Kisusi pamoja na Felister Nyambaya, walitokea Rorya.

Kutoka Wilaya ya Butiama, walioshinda ni Grace Bunyinyiga na Thabitha Idd, Abdalah Jumapili na Kananda Kananda walipitia Wilaya ya Musoma Mjini na katika Wilaya ya Tarime, walioshinda ni Mariam Mkono na Samson Gesase.

No comments: