Tuesday, October 16, 2012

Je Spika Makinda ni mgonjwa? uvumi wa afya yake waanza

Spika wa Tanzania Anne Makinda

Kumeanza kuwa na uvumi ambao bado haujathibitishwa rasmi na mamlaka za Serikali ya Tanzania kuhusu Afya ya Spika wa Tanzania Anne Makinda kwamba ni mgonjwa au la baada ya kuwepo habari kwamba amekwenda nchini  India kwa shuguli kikazi lakini pia  kwa ajili ya matibabu ya kawaida ya kucheki afya yake.

Tayari gazeti la Tanzania Daima la Tanzania leo limechapisha habari kwamba afya ya Spika huyo wa kwanza mwanamke nchini Tanzania inazua utata katika habari yenye kichwa cha habari  'AFYA YA SPIKA YAZUA UTATA" na kwamba huenda amelezwa katika hosptali ya Apollo nchini India.

Soma habari kamili hapa chini kama ilivyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima la leo Jumanne 16 October 2012

Bofya hapa usome kwa urefu habari hiyo kwenye gazeti la Tanzania Daima


No comments: