Monday, October 8, 2012

Kagera Sugar yaitafuna Yanga 1 - 0

Golikipa wa Kagera Suga, Hannington Kalyesubula aliyeudaka mpira huku beki wa Yanga, Nadir Canavaro akiutazama kwa makini kama utadondoka


Timu ya Yanga leo imejikuta ikipata kipigo cha bao 1 - 0  kutoka kwa wenyeji wao Kagera Sugar  katika mechi iliyofanyika leo katika uwanja wa Kaitaba mkoa Kagera

Bao la Kagera Sugar limepatikana kipindi cha pili cha mchezo dakika ya 25 ambalo limefungwa na mchezaji  Temmy Alfonce.

Hata hivyo Yanga walijitahidi kushambulia lengo la  Kagera Sugar lakini uimara wa mabeki wa timu haukuwapa nafasi ya kurudisha bao hilo hadi mpira unamalizika matokeo yakawa 1 - 0

No comments: