Monday, November 12, 2012

"CCM Dodoma Kanyage Twende!!!":Ujumbe NEC hapatoshi


Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wenzake katika Meza kuu jana wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM

Jakaya Kikwete akiingia kwenda kufungua mradi wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa CCM utakaokuwa na Hoteli ya kisasa ya nyota 5

Baada ya utaratabu mpya wa kuchagua wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM NEC kubadilika ambapo hupatikana kuanzia ngazi ya wilaya kumepunguza idadi ya Wajumbe wa NEC wa kupigiwa kura kura na mkutano Mkuu na sasa kumefanya mchuano uwe mkali zaidi tofauti na zamani.

Zamani Wajumbe wote wa NEC walikuwa wanapatikana kwa kupigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu lakini sasa ni wajumbe 10 tu kwa upande wa Tanzania Bara na 10 kwa upande wa Zanzibar ndio wanaopigiwa kura na mkutano Mkuu.

Kumekuwa na kampeni za chini kwa chini na nyingine za wazi wazi wagombea ambao baadhi yao ni vigogo wakijaribu kuwashawishi wajumbe wa Mkutano Mkuu wawapigie kura.

Yote kwa yote leo zitajulikana bichi na mbivu.

No comments: