Wednesday, November 28, 2012

Sharobaro Kumbe alitoa ahadi kabla ya kifo chake hiki hapa alichoahidi


“Masikini mdogo wangu, ametutoka akiwa mdogo, masikini mama yetu, ndoto za kujengewa nyumba na kuboreshewa maisha zimeishia barabarani,” ni maneno aliyokuwa akiyatoa dada wa marehemu wa mwaigizaji mashuhuri, Hussein Ramadhani ‘Sharo Milionea’ (27) aliyefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia jana.
   
.Dada huyo aitwaye Rehema Kadiri (38) alilieleza Mwananchi kuwa msanii huyo alikuwa akienda kijijini, Lusanga kumpelekea mama yake mzazi fedha kwa ajili ya kulimia shamba.

Alisema ahadi hiyo alikuwa ameitoa wiki iliyopita alipokuwa amekwenda kijijini hapo kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu babu yake, Mkieta Juma aliyefariki dunia mwaka juzi.
Mazingira ya ajali.
Hili ndilo gari lililoondoa maisha ya Sharobaro Billionea

Gari la mwigizaji hiyo lilipoteza mwelekeo na kupinduka mara kadhaa wakati akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda kijijini kwao, Lusanga mkoani Tanga, na kusababisha kifo chake saa 2.30 juzi usiku.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongiji cha Songa Kibaoni, Kijiji cha Songa, wilayani Muheza, Abdi Zawadi alisema ilipofika saa 2.30 usiku wakazi wa eneo hilo walisikia kishindo kikubwa ndipo wakaenda kushuhudia.

Alisema walipofika eneo la tukio, walikuta gari aina ya Harrier likiwa limepinduka, huku mwili wa mwanaume mmoja ukiwa pembeni, ndipo walipomfuata na kumkuta ameshakufa.
“Tulimtambua kuwa ni Sharomilionea baada ya kupekuwa mfukoni na kukuta kitambulisho cha mpiga kura kikiwa na jina la Hussein Ramadhani kikionyesha kuwa alijindikisha Lusanga, tukapaiga simu Kituo cha
Polisi Muheza na askari wakaja kuuchukua mwili.

Katika eneo la tukio ilishuhudiwa mti mkubwa aina ya mjohoro uliogongwa baada ya gari hilo kuachia njia, ukiwa umeanguka na gari kupinduka hadi umbali wa mita kama 50.
Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema ndani ya gari hilo lalikuwamo dereva peke yake, likiendeshwa kwa mwendo mkali, na baada ya kupinduka dereva huyo ambaye ndiye msanii Sharomilionea alitupwa nje.

Chanzo:Mwananchi