Tuesday, December 18, 2012

BREAKING NEWS!!!! Kimenuka Kariakoo risasi zarindima Mtu mmoja auawa


Baadhi ya watu waliojeruhiwa wakisaidiwa na Polisi wa kupambana ujambazi

 
 
 
 
 
 
Polisi wa kupambana na ujambazi (Picha zote kwa hisani ya blog ya michuzi)
 
 
 
Mtu mmoja ameuwawa  katika majibizano ya risasi yaliyotokea maeneo ya Msimbazi kariakoo, mtaa wa Livingstone kati ya Polisi na majambazi waliotaka kupora fedha zilizokuwa zinapelekwa benki ya NBC.

Majambazi hao waliokuwa wamevalia nguo za kiraia inasemekana walijua fedha hizo zinapelekwa leo hivyo walijiandaa kupora  ambapo Polisi nao waligundua hilo mapema hali iliyofanya majambazi hao kurusha risasi hovyo na kukimbia ili kukwepa kukamatwa.

Hadi sasa ni mtu mmoja anayeripotiwa kuuwawa .
 Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kwa kadri tutakavyokuwa tukizipata