Wednesday, December 19, 2012

Kaboyonga Mbunge wa zamani wa Tabora Amefariki

Marehemu Sijaru Kaboyonga
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema Mbunge wa zamani wa Tabora mjini  Siraju Juma Kaboyonga amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo jijini Dar  es Salaam.

Kwa mujibu taarifa zilizotolewa na Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF , Marehemu Kaboyonga  anatarajiwa kuzikwa kesho Alhamis na msiba upo nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam.

Marehemu ambaye alikuwa ni Mbunge wa zamani pia aliwahi kushika nyadhifa nyingine ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti ya Bodi ya Shirika la Hifadhi ya Jamiii NSSF na Meneja wa Kanda wa Benki ya East African Development Bank.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe AMEN. Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kwa kadri tutakavyoendelea kuzipata