Sunday, December 9, 2012

Majambazi yapora Maiti!!! Hii Kali


Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka mjini Morogoro kwenda mkoani Mara kisha kupora  takriban Sh19.8 milioni walizokuwa nazo waombolezaji.
Katika tukio hilo la kusikitisha lililotokea juzi mkoani Singida,  majambazi hao walivunja vioo vyote vya gari pamoja na jeneza lililokuwa na mwili wa Munchari Lyoba aliyekuwa mwanafunzi  wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) cha Morogoro na kumpekua marehemu.Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida, mkuu wa msafara uliokuwa ukisafirisha maiti,  Makaranga alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 7:30 usiku katika gari aina ya Land Cruiser mali ya SUA.

Akisimulia tukio hilo, Makaranga alisema kuwa lilitokea katika Barabara Kuu ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya Mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed Trans kuelekea mkoani Mara.  
Alisema kuwa gari hilo pamoja na jeneza, lililobeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne lilipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa barabarani na kuwalazimisha kusimama ndipo wakavamiwa na kundi kubwa la vijana, ambao walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.  

“Walipofika walipiga kioo cha gari letu kwa mbele na kumparaza kwa panga usoni dereva wetu. Baada ya hapo walivunja vioo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu tulichokuwa nacho,” alisema Makaranga.  
Makaranga alisema kuwa katika tukio hilo, aliporwa Sh2 milioni alizokabidhiwa azihifadhi kwa ajili ya kugharimia msafara huo, Sh8.8 milioni zilizochangwa na wanafunzi kama rambirambi kwa  mwenzao na jumla ya Sh9 milioni ambazo wasindikizaji walikuwa nazo mifukoni mwao.  

“Pia tuliporwa simu  zetu zote  za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu,” alisema.  
Makaranga aliyeeleza kuwa anafanya kazi za kiutawala SUA, aliwataja walioumizwa na majambazi hao kuwa ni pamoja na yeye, dereva wao na kiongozi wa wanafunzi, Idd Idd ambao walitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na kuruhusiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa amewasiliana na uongozi wa SUA ili watume gari lingine na kukarabati jeneza lililoharibiwa na majambazi hao.

Mlozi aliongeza kuwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi na Kamati ya Ulinzi na Usalama, watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa haraka iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.  
“Nimesikitishwa sana na tukio hili, inaelekea sasa binadamu tunaanza kutoka kwenye utu na kuhamia kwenye vitendo ambavyo binadamu wa Mwenyezi Mungu hawezi kuthubutu kuvifanya. Watu wanafikia hata kufungua jeneza na kuanza kulisachi,” alisema  Mlozi akionyesha masikitiko.

Alisema kuwa kwa sasa jeneza limefanyiwa ukarabati na  uongozi wa SUA umetuma gari jingine ili kuendelea na safari hiyo ya mwisho ya marehemu huyo.

Source: Mwananchi


4 comments:

oakleyses said...

chanel handbags, burberry outlet online, christian louboutin outlet, nike air max, oakley vault, tiffany and co jewelry, michael kors outlet online, michael kors handbags, burberry outlet online, ray ban sunglasses, michael kors outlet store, prada handbags, oakley sunglasses, kate spade outlet, christian louboutin shoes, michael kors outlet, longchamp handbags, christian louboutin, coach outlet store online, true religion outlet, louis vuitton outlet, longchamp outlet online, nike free, true religion, polo ralph lauren outlet, gucci handbags, louis vuitton handbags, coach outlet, louis vuitton outlet, prada outlet, nike air max, jordan shoes, nike outlet, polo ralph lauren, louis vuitton, longchamp outlet, red bottom shoes, tory burch outlet online, kate spade outlet online, michael kors outlet online, coach purses, ray ban outlet, michael kors outlet online, coach outlet, tiffany jewelry, cheap oakley sunglasses, louis vuitton outlet online

oakleyses said...

true religion jeans, sac louis vuitton, sac michael kors, vans pas cher, lacoste pas cher, timberland, chaussure louboutin, nike roshe, tn pas cher, true religion outlet, louis vuitton pas cher, nike air max, nike blazer pas cher, michael kors canada, nike air max, new balance pas cher, nike free, air max, sac vanessa bruno, hollister, mulberry uk, longchamp pas cher, ray ban pas cher, burberry pas cher, lululemon, nike air force, ray ban uk, ralph lauren, oakley pas cher, hermes pas cher, louis vuitton, air jordan, michael kors uk, nike roshe run, air max pas cher, north face, scarpe hogan, louis vuitton uk, nike free pas cher, longchamp, north face pas cher, hollister, ralph lauren pas cher, converse pas cher, barbour, guess pas cher, abercrombie and fitch

oakleyses said...

ferragamo shoes, soccer shoes, nike roshe, nfl jerseys, vans outlet, jimmy choo shoes, beats headphones, reebok shoes, valentino shoes, lululemon outlet, birkin bag, p90x workout, ugg outlet, asics shoes, mac cosmetics, longchamp, hollister, mcm handbags, ugg, babyliss, marc jacobs outlet, north face jackets, insanity workout, celine handbags, soccer jerseys, uggs on sale, canada goose outlet, wedding dresses, uggs outlet, replica watches, uggs outlet, canada goose, nike huarache, north face jackets, ugg boots clearance, mont blanc pens, instyler ionic styler, herve leger, nike trainers, canada goose outlet, canada goose outlet, giuseppe zanotti, new balance outlet, bottega veneta, ghd, ugg boots, chi flat iron, abercrombie and fitch, ugg soldes

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans