Tuesday, January 15, 2013

Jaji Mkuu na Spika watoa maoni ya Katiba Mpya

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto) akiongozwa na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu kutoka nje ya ukumbi katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Tume na Mahakama uliolenga kupata maoni ya mhimili huo kuhusu Katiba Mpya.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto) akitoa maoni ya Mahakama katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Wajumbe wa Tume, Makamau Mwenyekiti wa Tume na Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani, Prof. Mwesiga Baregu, Bi. Raya Suleiman Hamad na Bi. Jessica Mkuchu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo ambapo mhimili huo wa dola uliwasilisha maoni yake kwa Tume kuhusu Katiba Mpya. Wengine ni watumishi wa Bunge walioongozana naye.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (katikati) akiongea katika mkutano uliolenga kupata maoni ya wadau wa ulinzi kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto ni Mjumbe wa Tume na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.
 

No comments: