Tuesday, April 30, 2013

Real Madrid yatolewa Dortmund yaingia fainali


Pamoja na kushinda 2 - 0 timu Real Madrid ya Hispania jana iliyaaga rasmi mashindano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kutolewa kwenye mashindano hayo na timu ya Ujerumani ya Borusssia Dortmund kwa jumla magoli 4 -3.

Hii inafuatia kipigo cha mechi ya awali iliyochezwa nchini Ujerumani ambapo wakali hao wa Hispania ilikubali kichapo cha magoli 4 - 1 kutoka kwa Dortmund.



Leo ni mpambano mwingine wa kukata na shoka ambapo Barcelona wakiwa nyumbani nao watajaribu kujinasua dhidi ya Bayern Munich kutoka huko huko Ujerumani baada ya mechi ya awali kuchapwa na Bayern magoli 4 - 0.


Ili Barcelona waingie fainali itawalazimu kushinda magoli 5 - 0 au 4 - 0 ili wapigiane penati japo yachambuzi wa soka pamoja na kukiri lolote linaweza kutokea katika soka, lakini  wanaipa Barcelona nafasi ndogo ya sana ya kuingia fainali. Kwa mainti hiyo kuna uwezekano mkubwa timu mbili za Ujerumani zikakutana katika hatua ya fainali huko London mapema mwaka huu.