Sunday, May 12, 2013

Ulinzi mkali unatarajiwa makanisani leo baada ya mlipuko Arusha


Ulinzi mkali unatarajiwa kuimarisha leo katika makanisa mbali mbali hapa nchini kuafuatia mlipuko wa bomu uliotokea kule Arusha ambapo watu watatu walifariki na wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa vibaya.

Huenda ulinzi huo ukaimarishwa kufuatia ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa kule mkoani Arusha wakati alipokwenda kuwafariji waliofiwa kutokana na mlipuko huo pamoja na kuwapa pole majeruhi.

Rais Kikwete aliahidi  kuwa waumini wa dini mbali mbali wasiogope kumwabudu Mungu kwani serikali ipo na itahakikisha inatoa ulinzi.

Huenda hali ya ulinzi ikawa hivi katika baadhi ya makanisa hapa nchini.