Monday, August 26, 2013

Ni Dillish mshindi Big Brother Africa 2013

Kama ndoto lakini ndivyo ilivyokuwa usiku wa kuamkia leo ambapo mana dada raia wa Namibia Dillish ndiye aliyejinyakulia kitita cha dola 300,000 sawa na milioni 500 za kitanzania  baada ya kuwa mshindi katika onyesho la Big Brother Africa

Imewashangaza wengi maana mwana dada huyu alionekana asipewa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo hiyo lakani mambo yamekuwa tofauti na mawazo ya wengi.

Waliokuwa wanapewa nafasi kubwa tangu mwanzo ni Feza Kessy wa Tanzania, Melvin wa Nigeria, Oneal wa Botswana, Nando wa Tanzania na Angelo wa Afrika ya Kusini lakini bahati ikawa si yao kwani waliondolewa kabla ya fainali.

Feza Kessy aliyekuwa akipendwa na mashabiki kutokana na uchangamfu wake na urembo wake alijikuta akiangukia katika penzi la Oneal raia wa Botswana na kufanya apoteze umaarufu wake.

Wote Oneal na Feza Kessy waliondolewa na wenzao pamoja na mashabiki kutokana na kujitenga na wenzao na kuangalia mambo yao wakiwa ndani ya jumba hilo la Big Brother.