Sunday, August 4, 2013

Feza aponea chupu chupu abaki BBA, Oneal aaga rasmi

Mrembo Mtanzania anayeshiriki BBA Feza Kessy
Feza na mpenzi wake Oneal  kwenye jumba la BBA , na hata hivyo kufuatia kuingia kwenye mapenzi wawili hao walipachikwa jina la Oneza

Ni wazi sasa mamilioni yanamkaribia Mtanzania Feza Kessy ambaye anashiriki Big Brother Afrika baada ya usiku wa kuamkia leo kuponea chupu chupu kuyaaga mashindano hayo na badala yake mpenzi wake waliokutana katika jumba hilo Oneal ndiye aliyeyaaga mashindano hayo.

Kiuhalisia Feza ni tishio hata kwa housemate wenzake na tangu mwanzo walikuwa wakifanya kila mbinu ili aondoke lakini kutokana na kupendwa na watazamaji barani Afrika amejikuta leo akibaki kwenye jumba hilo.

Wengi waliona Feza Kessy asinge kuwa nominated kama sio kujiingiza kwenye mahusiano na Oneal kwenye jumba na kufanya achukiwe na washiriki wenzake na hata baadhi ya watazamaji. Hata hivyo bado inaonekana Feza ana nafasi kubwa ya kufanya maajabu kufika mbali kwani waliobaki sasa sio tishio kwake.

Waliokuwa kwenye kikaango wiki hii walikuwa ni Bimp kutoka Ethiopia, Feza kutoka Tanzania na Oneal kutoka Botswana.

Hivi ndivyo Afrika ilipiga kura na dada yetu kuponea chupu chupu

Hivi ndivyo Afrika ilivyopiga kura

Angola: Bimp 
Botswana: Oneal 
Ghana: Bimp 
Kenya: Feza
Ethiopia: Bimp 
Malawi: Bimp 
Namibia: Bimp 
Nigeria: Bimp 
South Africa: Oneal 
Sierra Leone: Feza
Tanzania: Feza
Uganda: Bimp
Zambia: Bimp
Zimbabwe: Bimp
Rest of Africa: Bimp 

Jumla: Bimp = 10, Feza = 3, Oneal = 2