Sunday, January 8, 2012

ANC yatimiza miaka 100


Maelfu ya raia wa Afrika ya Kusini wanaendelea na sherehe katika mji wa Bloemfontein kutimiza miaka 100 tangu chama cha ukombozi cha ANC kilipozaliwa.

Mapema leo kulikuwa na ibada iliyofanyika katika la Methodist karibu na Bloemfontein mahali ANC ilipoanzishwa kwa lengo la kupambana na utawala ya kibaguzi wa wazungu wachache.

Rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo Nelson Mandelea ameshindwa kuhudhuria sherehe hizo kutokana na hali ya kiafya.

Marais kutoka nchi za Afrika pamoja na watu maarufu akiwemo Askofu Desmond Tutu na mpigania haki za watu weusi nchini Marekani Jesse Jackson wanahudhuria sherehe hizo.

Mwenge maalum uliwashwa jana usiku kuadhimisha sherehe hizo.



No comments: