Vizuizi vya barabarani vimechomwa moto katika mji
mkuu wa Nigeria Lagos katika siku ya pili ya mgomo usio kuwa na kikomo
kufuatia kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.
Waandishi wanasema mji uko katika hali tete
baada ya mwandamanaji mmoja kuuawa mjini Lagos siku ya Jumatatu katika
maandamano yanayopinga pia kupanda bei maradufu ya mafuta.Biashara nyingi bado zimefungwa nchi nzima ikiwmeo mji mkuu.
Maandamano hayo yaliyoandaliwa na vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria unakaribia kuingia katika mji mkuu Abija ambako maduka, ofisi, shule, na vituo vya mafuta vimefungwa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP polisi walitumia mabomu yakutoa machozi kwa waandamanji wa Bauchi, mji ulio kaskazini. Hakuna majeruhi.
Mwandishi wa BBC Mark Lobel mjini Lagos anasema thamani ya biashara ya fedha katika maduka ya fedha nchini Nigeria ilishuka mara tano ya thamani yake Jumatatu, ingawa makampuni ya mafuta yanasema usafirishaji wa mafuta nje haukuathiriwa.
'Bahati mbaya'
Polisi waliomba kuwe na utulivu kwa baadhi ya waandamanaji waliochoma moto vizuizi barabarani, lakini kinyume chake walirusha mawe wakati maafisa wanazima moto huo, shirika la habari la AP liliripoti.Maelfu ya watu walioshiriki maandamano hayo rasmi mjini Lagos walitemea katika mitaa waifuata muziki wa sauti kubwa wenye midundo ya Afrobeat wakati mwingine askari wakipiga makofi na kupiga picha kwa mujibu wa AFP.
Wauza mafuta wa vidumu Nigeria wakinadi mafuta kwa madereva |
Mjini Kano, amri ya kupiga marufuku kutembea iliwekwa Jumatatu baada ya polisi kupambana na waandamanaji.
Maafisa wa vyama vya wafanyakazi walisema hakutakuwa na maandamano mengine mjini humo, lakini mgomo utaendela, mwandishi wa BBC Yusuf Ibrahim Yakasai anaripoti.
Gharama za mafuta na usafiri zimepanda maradufu baada ya ruzuku hiyo kusitishwa Januari 1, iliwakasirisha raia wengi ambao wanaona hiyo ndio namna pekee ya kunufaika na utajiri mkubwa wa mafuta nchini humo.
Wengi wa raia wa Nigeria wapatao milioni 160 million wanaishi chini ya $2 (£1.30) kwa siku, kwa hiyo kuongezeka ghafla kwa bei kumeongeza gharama za maisha zaidi.
Licha ya kuwa mtengenezaji mkubwa wa madini Nigeria haijawekeza katika miundombinu kusafisha mafuta kwa hivyo inaagiza mafuta mengi kutoka nje.
Wakati ruzuku ilikuwpoe , mafuta yalikuwa bei rahisi nchini Nigeria kuliko nchi jirani, kwa hiyo sehemu ya mafuta hayo ilikuwa ikisafirishwa nje kwa magendo.
Bei za mafuta Nigeria
- Bei ya vituo vya petrol wakati wa ruzuku: $0.40/ kwa lita
- Bei mpya kwa vituoni : $0.86Bei
- kabla kwenye soko la ulanguzi: $0.62
- Bei mpya kwenye soko la ulanguzi: $1.23
- Gharama ya ruzuku ya serikali kwa mwaka : $8bn
No comments:
Post a Comment