Waziri Mkuu Mizengo Pinda |
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameunda tume itayochunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni. Hata hivyo majina wajumbe wa tume hiyo bado hayajangazwa isipokuwa wanasema watatoka kwenye taasisi mbali mbali
Taarifa kamili ya Waziri Mkuu hii hapa chini
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI WA
KIDATO CHA NNE
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika
matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya
mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo
inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama
cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and
Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini
zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za
Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
Wadau
wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za
Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Amesema
Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla
watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, FEBRUARI 23, 2013.
No comments:
Post a Comment