Saturday, November 13, 2010

Aung San Suu Kyi aachiwa huru


Jeshi la Burma hatimaye limemwachia huru mwanasiasa maarufu na mtetezi wa demokrasia wa Burma.
Akionekana nje ya nyuma yake alipokuwa mjini Rangoon, Bi. Suu Kyi aliwaambia maelfu ya wafuasi wake kwamba washirikiane ili wafikie lengo lao la kisiasa.
Mwanasiasa huyo mshindi wa amani wa Nobel aliwekwa kizuizini mara 15 ndani ya miaka 21 iliyopita.