Thursday, November 18, 2010

Wabunge wa CHADEMA wasusia hotuba ya Rais Kikwete


Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo hii wamesusia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya ufunguzi wa Bunge jipya la Tanzania.
Wabunge hao ambao walikuwa ndani ya Bunge wakati rais Kikwete anaingia bungeni hapo walianza kutoka pale alikaribishwa kuhutubia bunge hilo.
Sababu kubwa inayoelezwa na CHADEMA kuamua kuchukua hatua hiyo ni kutomtambua Raisi Kikwete kwa madai kwamba hakuchaguliwa kihalali na kwamba matokeo yaliyompa ushindi hayakuwa halali.

No comments: