Sunday, November 14, 2010

Nani kuwa Waziri Mkuu Tanzania? je ni Mwanamke?


Baada ya Tanzania kupata Spika wa kwanza mwanamke Anne Makinda sasa macho na masikio ni kutaka kujua nani atateuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Waziri Mkuu.

Watu mbali mbali mashuhuri wameanza kutajwa miongoni mwao ni Mkurugenzi mtaafu wa makazi duniani Profesa Anne Tibaijuka.

Wanaompa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa waziri Mkuu kigezo wanachotumia ni uzoefu wa masuala ya kimataifa pia wa kuongoza.
Wakati wengi wakisuburi kujua ni nani atapewa nafasi hiyo nyeti zipo tetesi kwamba huenda nafasi ya naibu waziri mkuu iliyokuwepo wakati wa Serikali ya wa Awamu ya Pili ikarejea.

taarifa zilizopo ni kwamba huenda cheo hicho kutalenga katika kumpoza aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta ambaye jina lake lilienguliwa na kikao cha Kamati Kuu kilichoketi mjini Dodoma Jumatano wiki hii.

Habari zaidi zilisema Sitta aliitwa katika Ikulu ndogo mkoani Dodoma Ijumaa wiki hii na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Lengo la kuitwa katika mazungumzo hayo ni kujaribu kumpoza Sitta, ili akubali kupewa uwaziri katika wizara moja nyeti na unaibu waziri mkuu.

Hali hiyo ilimfanya Sitta kushindwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura lilofanywa
na Kamati ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alhamisi iliyopita (Novemba 1mwaka huu).

No comments: