Friday, December 10, 2010

Je Ouko aliuawa katika Ikulu ya Kenye?

Kuna taarifa kuwa mauaji ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Robert Ouko aliuwa kwenye moja ofisi za aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Daniel Arap Moi bunge la nchi hiyo limeambiwa.

Juhudi za uchunguzi wa mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1990 ambao ulifanyika karibu mara tatu hazikuzaa matunda na hii ni ripoti iliyoandaliwa na kuandikwa miaka mitano iliyopita.

Ripoti hiyo inataka uchunguzi zaidi ufanywe kwa viongozi wa juu akiwemo rafiki wa karibu wa rais Moi Nicholaus Biwott.

No comments: