Friday, December 3, 2010

Urusi kuandaa Kombe la Dunia 2018, Qatar 2022


Shirikisho la soka duniani, Fifa, limetangaza Urusi kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2018, baada ya kuzishinda nchi za England, Ureno na Uhispania, na Uholanzi na Ubelgiji.

Aidha Qatar nayo imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Nchi nyingine zilizokuwa zikiwania nafasi hiyo ni Australia, Marekani, Japan na Korea Kusini. (BBC Swahili)