Monday, January 23, 2012

BREAKING NEWS: Kenyatta na Ruto wana kesi


 Wawili waachiwa huru 

Mahamaka ya Kimataifa ya uhalifu ya The Hague Uholanzi ICC imewakuta  washtakiwa wanne wa machafuko ya kiasa nchini Kenye kuwa wana kesi ya kujibu.

Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta na Katibu wa Baraza la Mawaziri Fransis Muthaura sasa watashtakiwa kwa makosa dhidi ya binadamu ikiwa ni pamoja na makosa ya mauaji na utesaji.

Naye William Ruto na Joshua Arap Sang nao wamekutwa na kesi ya kujibu kuhusu machafuko hayo
Waliachiwa huru kwa kukosa ushahidi wa kutosha ni Mkuu wa Polisi wa zamani Mohamed Hussein Ali na Waziri wa Viwanda Hendry Kosgey.

Kenyatta ambaye alikuwa ni mfuasi wa Mwai Kibaki anadaiwa alishiriki machafuko hayo yaliyosababisha vifo vya watu zaidi 1,200  kuwaua na kuwabaka wafuasi wa Raila Odinga.

No comments: