Wednesday, January 4, 2012

Mchakato Kutaka Kumrithi Obama Moto


Mitt Romney
Barack ObamaWafuasi wa chama cha Republican wameanza kupiga kura ya kuwachagua wagombea watakaosimama kugombea kiti ya urais nchini Marekani.

Gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney amepata ushindi mwembamba katika uchaguzi uliofanyika katika jimbo la Iowa ikiwa ni hatua za mwanzo za kumchagua mgombea urais atakayepambana na  Rais wa Barack Obama anayetoka chama cha Democrat.

Uchaguzi huo umefanyika katika jimbo hilo ambapo pia utafanyika katika majimbo mengine yapatayo 50 ya Marekani katika miezi michache ijayo.
Mitt Romney katika harakati za kampeni

Romney amepata kama kura 8 zaidi ya akimshinda  Seneta wa jimbo la Iowa Rick Santorum.

Amepata kura 30,015 ya kura zote huku Santorum akimbulia kura 30,007

Ron Paul amekuwa wa tatu huku Newt Gingrich akishika nafasi ya nne.

No comments: