Sunday, December 11, 2011

Uganda Mabingwa wa CECAFA 2011


Wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda the Cranes wakifurahia na kombe la ubingwa wa CECAFA
 Timu ya Uganda umenyakua ubingwa wa Michuano ya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP mwaka 2011 baada ya kuifunga timu ya Rwanda katika mchezo wa fainali ulichezwa katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam Tanzania.

Uganda imeifunga timu ya Rwanda kwa penati 3 -2 baada ya kumaliza dakika 90 za kawaida zikiwa zimefungana 2 -2 ambapo ziliongwezwa dakika 30 ambazo nazo hazikuweza kumtoa mshindi.

Kipa wa Uganda Abby Dhaira ndiye aliyedaka penati ya mwisho ya Rwanda iliyopigwa na Ngabo Albert baada kumaliza ikiwa imepata penati 3 na kukosa 2. Rwanda ilipata penati 2 na kukosa 3.


Nahodha wa Uganda Cranes akipokea kombe la CECAFA kutoka kwa mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar Dr. Alli Mohamed Shein



Nahodha wa Uganda Cranes Andrew Mwesigwa

 Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) na Sudan, timu ya Sudan imeifunga Tanzania bara 1 - 0 na kunyakuwa nafasi ya tatu.

Kwa matokeo hayo timu ya Taifa ya Uganda ambao wamenyakua Ubingwa imepata kombe pamoja na kitita cha Dola za kimarekani 30,000 ambapo mshindi wa pili ambaye ni Rwanda imepewa dola 20,000 wakati mshindi wa tatu Sudan imenyakua dola 10,000.