Monday, October 22, 2012

BREAKING NEWS!!!!! Sheikh Farid mbaroni kwa uchochezi


Sheikh Farid Hadi Ahmed
Jeshi la Polisi Zanzibar limemtia mbaroni Kiongozi wa kundi la Uamsho Zanzibar na  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmed(41) ambaye alidai kutekwa na kupotea kwa siku tatu  pamoja na wenzake 64 wakiwemo viongozi sita wa kundi la Uamsho na Jumuiya ya Maimam Zanzibar kwa tuhuma za kuchochea ghasia na vurugu zilizosababisha  vitendo vya uporaji wa mali na uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Wakati wa vurugu Zanzibar palikuwa hapakaliki
Msemaji wa Polisi Zanzibar Insepekta Mohamed Mhina, amewataja viongozi waliokamatwa mbali na Sheikhe Faridi Hadi Ahmed(41) mkazi wa Mbuyuni wengine ni Sheikhe Mselem Ali Mselem(52) wa Kwamtipura  ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar.

Wengine ni Sheikhe Azan Khalid Hamadi(48) wa Mtendeni, Hassan Bakari Suleiman(39) wa Tomondo na  Ustaadh Mussa Juma Issa(33), Suleiman Juma Suleimain(66) pamoja na Mussa Juma Issa(37) wote wa Makadara mjini Zanzibar.  


 Inspekta Mhina amesema pamoja na kukamatwa kwa viongozi hao wa Jumuia mbili za Kidini mjini Zanzibar, Polisi pia imewakamata watu wengine sita kwa tuhuma za mauaji ya Askari Polisi.

Inspekta Mhina amesema viongozi waliokamatwa ni wale walikuwa wakihojiwa na Polisi tangu jana kwa lengo la kutafuta ukweli wa taarifa za kutekwa kwa Sheikhe Farid Hadi Ahmed kulikopelekea ghasia na uharibifu mbalimbali kabla ya kujitokeza tena hadharani juzi.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kamamishina wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa amesema kuwa Jeshi la Polisi Visiwani humo linaendelea na operesheni maalumu ya kuhakikisha kuwa kila aliyehusika katika ghasi hizo anakamatwa na kukabili mkono wa sheria.

Akizungumzia maendeleo ya Upelelezi wa Kesi ya Kuuawa kwa Askari Polisi CPL Said Abdarahaman Juma aliyeuawa usiku wa kuamkia Alhamis wiki iliyopita, Kamishna Mussa amesema Polisi wamefanikiwa kuwatia nguvuni watu sita kwa kuhusika na mauaji ya askari huyo.

Amesema hadi sasa Polisi inawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya askari huyo ambapo watuhumiwa watatu walikamatwa mjini Zanzibar na wengine watatu wamekamatwa mkoani Tanga.

Kamishna Mussa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Mohammed Said(35) wa Mwanyanya, Joli Gasuli(20) wa Vuga, Bakari Juma Yusufu(22) wa Mwembe Makumbi  na Amour Rished(40) wa Bububu ambao walikamatwa mjini zanzibar siku ya kwanza lilipotokea tukio hilo.

Amewataja watuhumiwa wengine ambao wamekamatiwa Mkoani tanga na ambao tayari wamesharejeshwa Zanzibar kuwa ni  Ali salum Seif(21) na Abubakari Haji Mbarouk(32) pamoja na mdogo wake Mohammed Haji Mbarouk(21) wote wakazi wa  Ndagaa mkoa wa Kusini Unguja.

Kamishna Mussa amesema Polisi bado inaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na wale watakaobainika kuhusika na mauaji ya askari huyo watafikishwa mahakamani.

Amesema kwa ujumla tangu kukamatwa kwa viongozi hao hali ya usalama katika mji wa Zanzibar imerejea upya na wananchi wameombwa kutoshabikia vitendo vyovyote vile vitakavyoweza kupelekea uvynjifu wa amani.

Amewataka Wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kshiriki katika mikusanyiko na kuwa chanzo cha fujo na kwamba kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo atashughulikiwa ipasavyo na mkono wa dola.

4 comments:

oakleyses said...

chanel handbags, burberry outlet online, christian louboutin outlet, nike air max, oakley vault, tiffany and co jewelry, michael kors outlet online, michael kors handbags, burberry outlet online, ray ban sunglasses, michael kors outlet store, prada handbags, oakley sunglasses, kate spade outlet, christian louboutin shoes, michael kors outlet, longchamp handbags, christian louboutin, coach outlet store online, true religion outlet, louis vuitton outlet, longchamp outlet online, nike free, true religion, polo ralph lauren outlet, gucci handbags, louis vuitton handbags, coach outlet, louis vuitton outlet, prada outlet, nike air max, jordan shoes, nike outlet, polo ralph lauren, louis vuitton, longchamp outlet, red bottom shoes, tory burch outlet online, kate spade outlet online, michael kors outlet online, coach purses, ray ban outlet, michael kors outlet online, coach outlet, tiffany jewelry, cheap oakley sunglasses, louis vuitton outlet online

oakleyses said...

true religion jeans, sac louis vuitton, sac michael kors, vans pas cher, lacoste pas cher, timberland, chaussure louboutin, nike roshe, tn pas cher, true religion outlet, louis vuitton pas cher, nike air max, nike blazer pas cher, michael kors canada, nike air max, new balance pas cher, nike free, air max, sac vanessa bruno, hollister, mulberry uk, longchamp pas cher, ray ban pas cher, burberry pas cher, lululemon, nike air force, ray ban uk, ralph lauren, oakley pas cher, hermes pas cher, louis vuitton, air jordan, michael kors uk, nike roshe run, air max pas cher, north face, scarpe hogan, louis vuitton uk, nike free pas cher, longchamp, north face pas cher, hollister, ralph lauren pas cher, converse pas cher, barbour, guess pas cher, abercrombie and fitch

oakleyses said...

ferragamo shoes, soccer shoes, nike roshe, nfl jerseys, vans outlet, jimmy choo shoes, beats headphones, reebok shoes, valentino shoes, lululemon outlet, birkin bag, p90x workout, ugg outlet, asics shoes, mac cosmetics, longchamp, hollister, mcm handbags, ugg, babyliss, marc jacobs outlet, north face jackets, insanity workout, celine handbags, soccer jerseys, uggs on sale, canada goose outlet, wedding dresses, uggs outlet, replica watches, uggs outlet, canada goose, nike huarache, north face jackets, ugg boots clearance, mont blanc pens, instyler ionic styler, herve leger, nike trainers, canada goose outlet, canada goose outlet, giuseppe zanotti, new balance outlet, bottega veneta, ghd, ugg boots, chi flat iron, abercrombie and fitch, ugg soldes

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans