Tuesday, November 27, 2012

Ndege nauli sawa na mabasi yazindua safari leo Tanzania




Ndege ya Fast Jet ikiwa tayari kwa safari ya majaribio

Abiria wakiwa ndani ya Ndege tayari kwa safari ya majaribio

Kitu angani
Abiria wa majaribio wakishuka kwenye ndege hiyo
Hatimaye ndege aina Fast Jet ambayo nauli yake ni sawa na mabasi ya mikoani imezindua rasmi safari zake leo nchini Tanzania katika mji wa Dar es Salaam.

Nauli ya ndege hiyo toka Dar es Salaam hadi Kilimanjaro kwenda na kurudi ni wastani wa Shilingi 86,000/-

Nauli hiyo itakuwa ndio nauli ya chini zaidi kwa safari ambapo kwa nauli ya chini kabisa bila kodi itakuwa ni  shilingi 32,000/-

Ndege hiyo inatarajiwa kuanza safari rasmi siku ya Alhmis ya Novemba 29.