Tuesday, November 13, 2012

Pigo TOT: Mariam Khamis hatunaye tena duniani!


MWIMBAJI nyota wa taarab nchini, Mariam Khamis aliyekuwa katika kikundi cha TOT Taarab, amefariki dunia katika hospitali ya Muhimbili baada ya kujifungua. Mariam alijiunga na TOT akitokea katika kundi la  Five Stars Modern Taarab.
 
Mariam, ambaye aliwahi kutamba kwa kibao chake cha ‘Paka mapepe’,  mbali na kuimbia kundi la Five Stars, Mariam pia aliwahi kung’ara alipokuwa katika vikundi vya East African Melody na Zanzibar Stars.Baadhi ya vibao alivyotamba navyo katika vikundi hivyo ni pamoja na ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe! Amina

No comments: