Wednesday, December 5, 2012

Breakingi News!!!! Ajali mbaya yaua Watu wa Familia Moja




B

Baadhi ya watu wakishuhudia miili ya watu waliofariki kwenye ajili hiyo ili kuwatambua

Ajali  mbaya  imetokea  mkoani Iringa mchana  wa  leo na kusababisha  vifo  vya  watu  wanne  wa familia  moja  pamoja na mfanyakazi  wa ndani.

Ajali  hiyo  imetokea katika  eneo la Tanangozi  wilaya ya  Iringa kwenye kizuizi cha barabara  cha mafundi wa kutengeneza barabara  kuu ya Iringa -Mafinga  mkoani Iringa mida ya saa nane mchana

Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4  lenye namba  za usajili T 770 BMP kuliparamia lori  lenye tela kwa nyuma.  Huku  chanzo kikitajwa  kuwa ni kuendesha  kwa mwendo kasi  wa  dereva  wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke  na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.

Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo   chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha  kwa mwendo kasi na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa  gari hiyo ilikuwa ikitokea  jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.

Hivyo katika ajali  hiyo  abiria  wote  wanne akiwemo baba na mama  wa  watoto  wawili  waliokuwemo katika gari  hiyo pamoja na  watoto hao  kufa papo hapo na maiti  zote  kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.

Majina ya  waliokufa  ni pamoja  na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva  wa gari hilo na baba  wa familia  hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi  wao  wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel  huku majeruhi katika ajali  hiyo ni mmoja na amekimbizwa  Hospital ya mkoa  wa Iringa.