Sunday, July 10, 2011

Sudan ya Kusini taifa jipya barani Afrika


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ampongeza:


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akimpongeza Rais wa Sudan mpya ya Kusin Generali Salva Kiir Mayardit mara tu alipaapishwa kuwa rais wa Sudan ya Kusini

Hatimaye Sudan ya Kusini imepata uhuru wake na sasa ni taifa jipya duniani likiwa la 54 barani Afrika. Huenda siku ya Jumamosi ya Julai 9, 2011 itaendelea kukumbukwa kama siku ya uhuru wa taifa hilo ambalo sasa litakuwa likijiendeshea mambo yake yenyewe.

Generali Salva Kiir Mayardit aliapishwa rasmi kuwa rais mpya wa Sudan ya Kusini huku akishuhudiwa na marais wapatao 13 akiwepo rais wa Tanzania Jakaya Kikwete. Hata hivyo changamoto kubwa inayolikabili taifa hili jipya ni umaskini pamoja na uduni wa huduma za jamii kama elimu , maji na huduma za afya.

Rais Kiir Mayardit sasa ana changamoto kubwa ya kuijenga nchi hiyo ambayo pia ina rasimali nyingi yakiwemo mafuta. 

Rais Jakaya Kikwete akifurahi na Rais mpya wa Sudan ya Kusin Generali Salva Kiir Mayardit

Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Sudan ya Kusin Salva Kiir Mayardit wakizungumza bila shaka Kikwete anamwambia "kuzaa sio kazi kazi kulea mwana"

Mke wa Rais Kikwete Mama Salma akipokea ua mara tu Rais Kikwete na mkewe walipowasili katika uwanja wa ndege wa Juba tayari kuhudhuria sherehe za kuanzishwa kwa taifa jipya la Sudan ya Kusini


No comments: