Tuesday, December 18, 2012

Ndege yaanguka Katavi rubani anusurika kifo, ajeruhiwa






RUBANI wa ndege ndogo mali ya TANAPA,  Athuman Bujwanga (47) mkazi wa Mahale Kigoma amenusurika kifo baada ndege hiyo aliyokuwa akiiendesha kupata hitilafu ikiwa hewani na kuanguka kando ya Mto Nsemulwa nje ya mji wa Mpanda Mkoani Katavi .


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo .


Alisema kuwa ndege hiyo aina ya Cessna yenye uwezo wa kubeba abiria wanne yenye namba za usajiri 5H F25C 182 ilianguka umbali wa kilometa moja kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda uliopo Kashaulili muda mfupi baada ya kupaa, ikiwa njiani kuelekea Mlele katika mbuga ya Taifa ya Katavi kujaza mafuta.
 

Ndege hiyo ilifika Mpanda ikiwa na abiria mmoja ikitokea Tabora na kisha baada ya kumshusha abiria huyo iliruka kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kujaza mafuta ili iweze kurejea Tabora.

Mmoja wa  walio shuhudi tukio  hilo  Credo Mwanisenga, alieleza  kuwa wakati   akiwa  anafanya shughuli  zake  za kilimo  ghafla  aliona  ndege  iliyo  kuwa  angani  ikizimika  na kisha  baada ya  muda  mfupi   ikaanguka   jirani  na mti wa mwembe.  Mara, walifika katika eneo hilo  kwa lengo la kutoa msaada. Iliwachukuwa muda  kuanza kutoa msaada  kwa  rubani huyo  aliyekuwa ndani ya ndege  peke yake,  kutokana  na eneo hilo kuwa na nyuki wengi  ambao walianza kuwashambulia waokoaji hao.

Hata hivyo  waliewza  kufanikiwa kumtoa  rubani  huyo   huku akiwa  amepata  majeruhi makubwa sehemu ya  uso wake  na maumivu  sehemu ya kifua hali akikohoa damu. , rubani huyo alipewa msaada na wananchi waliokuwa wakifanya shughuli zao za kilimo kwenye mashamba yao karibu na eneo ilikotokea ajali, na alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya mjini Mpanda kwa gari la Meneja wa Uwanja wa Ndege aliyefika kwenye eneo la tukio, ambapo alishonwa nyuzi nane katika paji lake la uso na hatimaye aliruhusiwa kurejea nyumbani.
 

Naye Meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda, Mahamud Muhamed  alisema  ajali  hiyo  ilitokea jana  majira ya  saa 10  na dakika 55 jioni  katika  kijiji  cha Nsemlwa wilayani hapo.

Ndege hiyo imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.

Muhamed alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo   cha ajari  hiyo  kilitokana na    njini ya ndege  hiyo  kufeli wakati ikiwa angani, hata hivyo uchunguzi wa kina kuhusiana na ajali hiyo bado unaendelea.