Monday, December 17, 2012

Simbacheawene naye Moto aionya TANESCO, Marufuku nguzo kutoka nje


SERIKALI imepiga marufuku Shirika la Umeme Tanzania (Tanaesco) kununua nguzo za umeme kutoa nje ya nchi.
Katika marufuku hiyo, imeeleza kuwa kitendo cha kutoa tenda kwa kampuni za nje na kuacha za ndani ya nchi zinazozalisha nguzo hizo ni cha aibu kwa taifa.



Akizungumza baada ya kufanya ziara ya siku moja ya kikazi, Naibu Waziri wa Nishari na Madini, George Simbachawene alisema kuanzia sasa nguzo za umeme hazitaagizwa kutoka nje kutokana na viwanda vya ndani kuzalisha nguzo zinazotosheleza.

Alisema kitendo cha kuagiza nguzo nje ni matumizi mabaya ya fedha za umma, kwani kinaongeza gharama za bidhaa hiyo hapa nchini na kuua viwanda vya ndani.Alisema kimsingi Tanzania ilistahili kuuza nguzo nje ya nchi na si kununua na kwamba kitendo hicho kinaingizia Serikali na wananchi wake harasa kubwa.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo baada ya viongozi wa viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme vya Green Resouces na Sheda General Suplies LTD vyote vya  wilayani Mufundi mkoani hapa kueleza kuwa kampuni zinazouza nguzo hapa nchini zimekuwa zikinunua nguzo toka katika viwanda vyao.

Imeelezwa kuwa nguzo zinazotumiwa na shirika hilo huagizwa kutoka nje ya nchi ikiwamo Kenya na Afrika ya Kusini kwa madai kuwa nguzo za hapa nchini hazina ubora na hazitoshelezi.

Source: Mwananchi

No comments: