Sunday, February 17, 2013

Padri auawa kwa kupigwa risasi Zanzibar akielekea kusalishaMarehemu Padri Evaristus Mushi
Padre wa Kanisa la Katoliki la parokia ya Minara Miwili lililopo mji mkongwe, Padri Evarist Mushi amefariki Dunia baada ya kupigwa risasi utosini na watu wasiojulikana.

Padri huyo alikuwa akielekea kuendesha misa ya saa 3 asubuhi hii kwenye kanisa la Mt. Theresia na akiwa eneo la Mtoni alisimamishwa na watu wawili ambapo mmoja wao alimpiga risasi utosini na kufariki papo hapo,mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali kuu ya Zanzibar iliyopo Mnazi Mmoja.

Hili ni tukio la pili  kwa Mapadri kushambuliwa huko Zanzibar ndani ya kipindi cha miezi miwili. Mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa hukusika na tukio hilo
Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kwa kadri tutakavyokuwa tunazipata endelea kuwa nasi

No comments: