Sunday, February 17, 2013

Pinda mgogoro nani achinje Wakristo au Waislamu wamtoa jasho

 

IMG_0122
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.

Bucha ya Wakristo ambayo ndio chanzo cha mgogoro

IMG_0143
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Ahmed Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa Buswelu, Athumani Ali katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza. (Picha zote na habari kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu)
Sakata la nani achinje nyama kati ya Waislamu na Wakristo bado linaumiza vichwa, ambapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja nyama yaendelee, hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.

Kufuatia hali hiyo, Pinda ameagiza kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kwamba kazi hiyo ifanyike haraka iwezekanavyo, na kisha ripoti yake iwasilishwe Serikalini kwa hatua zaidi za kimaamuzi.

Waziri Pinda ameyasema hayo muda mfupi uliopita leo, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, kuhusiana na kikao chake cha pamoja na viongozi wa Kikristo na Kiislamu, kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la Mwanza, kwa lengo la kutatua mgogoro wa kidini unaoonekana kuota mizizi.

Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda, imekuja siku chache baada ya kutokea mapigano makali baina ya wafuasi wa dini ya Kiislamu na Wakiristo kuzuka huko Buseresere-Katoro katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, ambapo mchingaji mmoja aliuawa kwa kuchinjwa huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya.

Aidha, Pinda alikemea vikali vurugu za kidini zilizotokea mkoani Geita, na kuwataka viongozi wa madhehebu yote ya dini kuheshimiana, kujenga mshikamano na kutohasimiana, kwani wao ni watu muhimu sana katika maendeleo na utulivu wa nchi.
IMG_0077
Sheikh Hasani Kabeke wa Mwanza akichangia katika kikao cha klutatafuta muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji wanyama kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Banki Kuu jijini Mwanza.
IMG_0084
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza. IMG_0094
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza.IMG_0102
Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza .(Picha na habari ni kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: