Wednesday, March 6, 2013

Mhariri Abasolom Kibanda aliyejeruhiwa apelekwa Afrika ya Kusini

Wafanyakazi wa ndege maalum ya kukodi wakimwingiza kwenye Absalomu Kibanda

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absalomu Kibanda amesafirishwa kwenda Afrika ya Kusini kwa matibabu za zaidi kufuatia kujeruhiwa vibaya hapo jana na watu wasiojulikana.

Awali Bwana Kibanda alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hosptali ya taifa ya Muhimbili.

Kibanda amejeruhiwa vibaya kichwana na amepasuliwa jicho lake la kushoto.