Tuesday, March 12, 2013

Uchaguzi wa Papa waanza Pengo anaweza kuwa Papa

Mudhama Policap Kardinali Pengo (kulia)  leo  hii akiwa na Makardinali wenzake Vitican City


Mudhama Policap Kardiali Pengo kushoto akiwa na mmoja wa makardinali hapo jana mjini Vatican

Zoezi la kumchagua papa atakayeongoza kanisa Katoliki duniani limeanza Vatican City kwenye jumba maarufu la Sistine Chapel ambalo hutumika kwa ajili hiyo.
Makardinali wapatao 115 akiwepo Mudhama Policarp Kardinali Pengo wa Tanzania ni miongoni mwa walikusanyika kufanya zoezi hilo.
Yoyote kati ya makardinali hao anaweza kuwa papa mpya hivyo Kardinal Pengo naye ana nafasi ya  kuwa papa mpya baada ya Papa Benedict xiv ambaye amestaafu.
Kwa sasa Papa Benedict amepewa jina jipya na ataitwa Papa Emaritus au Papa Emeritus wa Roma. 
Kinachosubiriwa hapo kwa sasa ni moshi mweupe ambao ndio utakaonyesha papa mpya amepatikana na kama hajapatikana baada ya kupiga kura moshi mweusi utaonekana.
Makardinali hao watakaa katika jumba hilo hadi papa apatikane. Hawaruhusiwi kuwasiliana na mtu yoyote na watakuwa wakipiga kura mara nne kwa siku.