Friday, April 12, 2013

Mbunge ataka bangi iruhusiwe, mwingine ataka wanaume wafundishwe kutongoza


Leticia Nyerere
Ally Kessy
Mbunge wa Nkasi Ali Kessy ameitaka serikali iruhusu raia wa Tanzania walime bangi ili wapate fedha za kigeni.

Mbunge huyo alikuwa akiuliza swali la nyongeza ambapo alimuuliza Naibu Waziri wa Kilimo

Wakati mbunge huyo akitaka hayo mbunge mwingine wa viti maalum Leticia Nyerere naye ametaka serikali ianzishe kituo maalum cha kufundisha wanaume kutongoza wanawake ili kupunguza vitendo vya kuwabaka walemavu.

" Kwa kuwa wanaume wengi wanaowabaka walemavu wengi wao wana matatizo ya akili na hawajimiani na hivyo kushindwa kuwashawishi wanawake wazima. Je serikali haioni kwamba ipo haja kuanzisha kituo za kuwafundisha wanaume ili waweze kujiamini na kuachana na ngono ya dezo " aliuza Mbunge huyo

Mbunge huyo alikuwa akiuliza swali la nyongeza.

Hata hivyo serikali katika majibu yake imesema hayo hayawezekani