Thursday, May 2, 2013

Barcelona yala kipigo cha mbwa mwizi yafungwa tena na Bayern 3 - 0


Siku ya jana ilidhihirisha kuwa ligi ya bundersliga ya Ujerumani haikamatiki baada Barcelona kwa mara nyingine kutoka Hispania kupata kipigo cha paka mwizi kama sio mbwa mwizi baada kwa mara nyingine kufungwa magoli 3 - 0 katika mchezo wa nusu fainali ligi ya mabingwa Ulaya na kuwaacha Bayern Munich wakitinga fainali kwa jumla ya magoli 7 - 0.

Kwa maana sasa kombe wa vyovyote litakwenda Ujerumani  baada ya Borussia Dortmund nayo kutoka ujerumani hapa juzi kuingia fainali kwa kishindo. Sasa Bayern watakutana na ndugu zao Dortmund katika fainali ya mashindano hayo baadae nchini Uingereza

  

No comments: