Lori lenye namba za usajili T 532 AJF lililopata ajali na kuua watu wanakadiriwa kufikia 14 Chunya mkoani Mbeya. |
WATU wanaokadirikwa kufikia 14 wamefariki dunia na wengine 41 kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Mitsubish Fuso waliyokuwa wakisafiria kutoka mnadani wilayani Chunya mkoani Mbeya kusini mashariki mwa Tanzania kupinduka.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Anacret Malindisa, tukio hilo lilitokea Septemba 24 mwaka huu majira ya 9;30 alasiri katika eneo la kijiji cha Msangamwelu wilaya ya Mbeya vijijini barabara ya Chunya-Mbeya.
Taarifa zinasema watu 11 walifariki dunia papo hapo, ambapo miili yao ilipelekwa katika Hospitali za Rufaa Mbeya na ile Teule ya Mbeya Vijijini ya Ifisi.
Mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo akipatiwa matibabu |
Kamanda Malindisa aliwataja waliofariki papo hapo ambao walitajwa kwa kila moja kwa jina moja kuwa ni Exzavery, Kaloli, Lembo, Masai, Kashinje, Noa,mama Anna Ugalahenga, Mwakalasya, Meshack na Mwakilasa ambao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Malindisa alisema majeruhi 37 wamelazwa katika Hospitali ya Teule ya Ifisi wakati majeruhi wengine wanne wanatibiwa katika hospitali ya Mwambani iliyopo mji wa Mkwajuni wilayani Chunya.
Naye Muuguzi Mkuu wa hospitali teule ya Ifisi Rhoda Kasongwa amewataja waliofariki baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo, kuwa ni Emilia Mwangove (40), mkazi wa Mbalizi, Grasiano Kalinga (37) na Msafiri Tinda (35) wote wakazi wa Mwanjelwa mjini Mbeya.
Aidha amewataja majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo ya Ifisi kuwa ni Mussa Mwangowe (27),Juma Mwambene (24),Msafiri Msangawale (20),Nelson Mwanyakule (45), Enock Saimon (28),Daudi Sanga (32),Aliko Mwakanjwanga (36), Daudi Joramu (3) Juma Mwakatobe (25), Satieli Kiwasi (45), Stany Elias (23) , na Charles Sanga (33).
Wengine ni Mussa Ezekiel (27), Stwen Mwaibeju (25), Maiko Siwale (30), Estron Chaula (21),Amina Mwanyakule (42),Mbonis Kapoka (27) na Atu Mnkwama (63) wote wakazi wa Mbalizi.
Majeruhi wengine waliolazwa katika hosptali hiyo ni Amani Emanuel (23) mkazi wa Songwe, Aneth Asangalwisye (43) mkazi wa Ilemi, Kachele Kasekenya (36) mkazi wa Mwanjelwa, David Mwakalasya (52) mkazi wa Air port, Nico Kessy (22) mkazi wa Utambalila,Leonard Paul (41) mkazi wa Ilemi, Daudi Sanga (29) mkazi wa Air port, na Likugulan Lolamatu (35) mkazi wa Uhindini,
Muuguzi Mkuu huyo amewataja wengine kuwa ni obart Mwalyambi (25) mkazi wa Makunguru, Adreano William (33) mkazi wa Mwanjelwa na Jenipher Mafupa mkazi wa Mwanjelwa.
Majeruhi wengine ni Aneth Kajenga (43) mkazi wa Ilemi, Fausta Ndelwa (26) mkazi wa Iyunga,Hadija Hussein ( 42) mkazi wa Chunya, Ikupa Nobwa (39) mkazi wa Chunya,Victor Sondanki (42) mkazi wa Mbeya,Hilda Juma (40) mkazi wa Mbeya na Lukia Andrea (23) mkazi wa Air port.
Bi Rhoda aliwataja majeruhi watatu ambao hali zao ni mbaya na wamehamishiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya kuwa ni Amina Mwanyakule, Aneth Kajenga na Eliud Kalekenya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya alisema gari hilo lenye namba za usajili T 532 AJF lililokuwa ikiendeshwa na Kasenti Kapusi lilipinduka na kuacha njia baada ya dereva wake ambaye ndiye mmiliki wa gari hilo mkazi wa Iwambi jijini Mbeya kumshinda kukata kona .
No comments:
Post a Comment