Baadhi ya watu wakitia sahihi kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha mwanaharakati maarufu wa mazingira Marehemu Wangari Maathai |
Watu mbali mbali duniani wanaendelea kutuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha aliyekuwa mwanaharakati maarufu wa mazingira duniani na Mtunukiwa wa tuzo ya Amani ya Nobel Prof Wangari Maathai ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia siku jumatatu.
Marehemu Wangari Maathai enzi za uhai wake |
Profesa Wangari Maathai alipata tuzo la amani ya Nobel mwaka 2004, kufuatia juhudi za kupigania uhifadhi wa mazingira nchini Kenya.
Mbali ya kuwa Mwanaharakati wa Maswala ya Mazingira na haki za binadamu , Wangari Maathai pia alikuwa mwanasiasa shupavu. Amewahi kuhudumu kama Mbunge na Naibu waziri wa Mazingira nchini Kenya.
Prof Maathai pia katika uhai wake alipata tuzo mbalimbali za kimataifa kwa kutambua mchango wake.
Alipendwa na watu duniani hapa yupo na Rais wa sasa wa Marekani Barak Obama |
Prof. Wangari Muta Maathai alianzisha vuguvugu la Green Belt mnamo mwaka 1977, ambapo alifanya kazi na wanawake kote nchini kuboresha maslahi yao na kuhifadhi mazingira.
Alikuwa mtetezi mashuhuri wa matumizi bora ya mali asili . Shughuli zake zilitambuliwa mara kwa mara kote duniani.
Marehemu ameacha watoto watatu, wawili wakiume na mmoja wa kike.
Mchango wake katika harakati za mazingira utakumbukwa daima hapa akipokea tuzo ya Nobel |
2 comments:
qzz0521
supreme clothing
ferragamo outlet
christian louboutin outlet
true religion jeans
swarovski outlet
michael kors outlet
cleveland cavaliers jersey
moncler outlet
canada goose outlet
wizards jerseys
WWW0620
michael kors outlet
valentino outlet
jordan shoes
puma outlet
saucony shoes
kobe bryant shoes
longchamp handbags
pandora jewelry
michael kors handbags
futbol baratas
Post a Comment