Wednesday, July 13, 2011

Breaking News: Rostam ajivua 'gamba' ndani ya CCM

Rostam Aziz


Mbunge wa Igunga Rostam Aziz amejiuzulu nyadhifa zote ndani ya Chama Cha Mapinduzi ikiwemo nafasi ya Ubunge.

Kwa mujibu wa Shirika la habari za Utangazi Tanzania TBC1 Rostam ametangaza hatua hiyo akiwa jimboni kwake Igunga mkoani Tabora.

Rostam anasema kuwa ameamua kuchukua hatua baada ya kushauriana na familia yake na amesema ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa chama chake.

Amesema sababu kubwa ya kujiuzulu nafasi hizo inafuatia chama cha Mapinduzi kutaka baadhi ya wanachama wenye tuhuma kujiuzulu nyazifa walizonazo ndani ya chama katika muda wa siku 90 tangu walipokutana mkoani Dodoma miezi mitatu iliyopita.

Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kwa kadri tutakavyokuwa tunazipata.

No comments: