Friday, July 22, 2011

Jairo anatembelea uzi mwembamba, ateuliwa wa kumkaimu

Eliakim Chacha Maswi
Hatimaye nafasi ya David Jairo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini imepata mtu wa kuiziba kwa muda kufuatia Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L. Luhanjo,  kumteua Eliakim Chacha Maswi kukaimu nafasi hiyo.
Taarifa ya Ikulu inasema: "Kufuatia Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Bwana David K. Jairo, kupewa likizo kwa muda, Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L. Luhanjo, amemteua Bwana ELIAKIM CHACHA MASWI, kuwa KAIMU KATIBU MKUU, Wizara ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 22 Julai, 2011."
          Bwana MASWI, kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.