Sunday, November 18, 2012

Serengeti Boys yaitambia Congo Brazaville yaichapa 1 - 0 Timu ya Taifa  ya Tanzania chini ya miaka 17 Serengeti Boys imeifunga timu  ya Taifa ya Congo Brazaville goli  1-0.

Goli hilo pekee limefungwa na Mudathiri yahya Abbas dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza baada ya kutokea faulu na kupigwa mpira wa adhabu ambao aliutumbukiza moja kwa moja ndani ya wavu kutoka umbali wa takribani meta 21.
Serengeti Boys walipewa adhabu hiyo badaa ya mabeki wa timu ya Congo kumchezea rafu mshambuliaji  Hussein Twaha Ibrahim  alipokuwa akikatika katika msitu wa mabeki wa timu hiyo ya Congo Brazaville.

 Timu hizo itarudiana tena baada ya wiki mbili zijazo nchini Congo Brazaville.

No comments: