Friday, November 2, 2012

Serikali yachunguza Vigogo walioficha fedha Uswis

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda
 Serikali ya Tanzania imeanza kufanya uchunguzi wa kina ili kujua ukweli na kuwachukulia hatua watu wote walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema bungeni jana kuwa, mara baada ya uchunguzi huo kukamilika Serikali itatoa taarifa kuhusu uchunguzi huo.

Pinda alikuwa akijibu swali aliloulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu jana asubuhi.
“Jambo hili kwa uzito wake, tumeanza kulifanyia uchunguzi ili kujua ukweli wake na hatua stahiki za kuchukua, tukimaliza tutatoa kauli kama ilivyo kawaida yetu, “ alisema.



Mbowe katika swali lake alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kuhusu taarifa za kuwapo kwa mabilioni ya fedha katika akaunti za benki mbalimbali nchini Uswisi ambazo zimewekwa na baadhi ya vigogo serikalini na viongozi wastaafu.

Katika Bunge la Bajeti lililopita, Kambi ya Upinzani ililiibua suala hilo wakati wa hotuba yao ya Bajeti wakieleza kuwa kuna jumla ya Sh360 bilioni zilizofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

Taarifa kutoka Benki Kuu ya Uswisi inaonyesha kuwa baadhi ya  fedha hizo zimewekwa katika akaunti za vigogo hao na kampuni za mafuta na gesi zilizopo nchini.

Jumanne wiki hii,  Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alipokuwa akichangia azimio la kuridhia marekebisho ya pili ya Mkataba wa Ushirikiano kati ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP), alisema Serikali iutumie ushirikiano huo kurejeshwa mabilioni yaliyofichwa nchini Uswisi.

Naye  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara Rombo, mkoani Kilimanjaro Oktoba 26 mwaka huu, alimlipua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hoseah, akidai kuwa bosi huyo ameandika barua Uswisi, akieleza kwamba Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki za nchini hiyo.
Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha akisema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.

2 comments:

oakleyses said...

ferragamo shoes, soccer shoes, nike roshe, nfl jerseys, vans outlet, jimmy choo shoes, beats headphones, reebok shoes, valentino shoes, lululemon outlet, birkin bag, p90x workout, ugg outlet, asics shoes, mac cosmetics, longchamp, hollister, mcm handbags, ugg, babyliss, marc jacobs outlet, north face jackets, insanity workout, celine handbags, soccer jerseys, uggs on sale, canada goose outlet, wedding dresses, uggs outlet, replica watches, uggs outlet, canada goose, nike huarache, north face jackets, ugg boots clearance, mont blanc pens, instyler ionic styler, herve leger, nike trainers, canada goose outlet, canada goose outlet, giuseppe zanotti, new balance outlet, bottega veneta, ghd, ugg boots, chi flat iron, abercrombie and fitch, ugg soldes

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans