Thursday, November 1, 2012

BREAKING NEWS!!!!!!! Polisi yasema maandamano ya Waislamu kesho Marufuku
Mmoja Askari Polisi Mahakamani Kisutu leo
 Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema litamchukulia hatua kati yoyote atakayeandamana kesho kufuatia baadhi ya Waislamu kutangaza kuwa kesho watafanya maandamano makubwa.

Waislamu hao wanashinikiza Katibu wa Taasis za Kiislamu Sheikh Issa Ponda ambaye ana kesi mahakamani kuachiliwa kwa dhamana.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleimani Kova amesema maandamano hayo yamepigwa marufuku na kwamba Polisi na vikosi vingine vya usalama vimejiandaa kukabiliana na yeyote atakayejaribu kufanya maandamano hayo

Leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mji Dar es Salaam Askari wa Jeshi la Polisi waliweka ulinzi mkali wakati Sheikh Ponda alipopelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili ambapo pia mahakama imemnyima dhamana kwa sababu zinazoelezwa na kuwa ni maslahi ya taifa na usalama wa nchi.

Polisi wa Kikosi cha Mbwa tayari kwa lolote leo
Sheikh Issa Ponda

No comments: