Monday, March 18, 2013

Manumba apoteza fahamu siku 42, sasa apata nafuu



Robert Manumba
Mkurugen-zi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba amezung-umzia ugonjwa wake ambao ulisababisha kutojitambua kwa siku 42 na kwamba sasa anaendelea vizuri.
Kwa sasa Manumba ambaye amelazwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu, anaendelea vizuri na sasa anafanya mazoezi mepesi ya kusimama na kutembea kama sehemu ya matibabu yake.

" Kwa sasa ninashukuru naendelea vizuri, nina-washukuru madaktari wa hapa ambao wamejitahidi maana ni kama watu wal-ishakata tamaa kwamba siwezi kupona,” alisema Manumba alipozungumza na Mwananchi katika Hos-pitali ya Millpark alikolazwa jijini Johannesburg.
Alisema tatizo kubwa lili-lokuwa likimkabili ni ugon-jwa wa malaria kwani ali-popimwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikutwa na wadudu wa ugonjwa huo 500.
“Yaani huwezi kuamini, nilikuwa na wadudu 500 lakini nilikuwa naendelea na kazi tu kama kawaida, sasa tiba ya malaria ndiyo ilisababisha kuibuka kwa magonjwa mengine lukuki ambayo yalisababisha nisiji-tambue kwa siku 42,” alise-ma Manumba.
Manumba anasema ni kwa mkono wa Mungu amepa-ta nafuu kubwa baada ya juhudi kubwa za madaktari katika kupigania uhai wake.
Alipelekwa Afrika Kusini Januari 23, mwaka huu baa-da ya kupata nafuu kidogo.
Alisema anawashukuru madaktari wote walio-hangaika usiku na mchana katika hospitali alizolazwa kuanzia Muhimbili na Aga Khan, jijini Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwa ndege maalumu hadi Johan-nesburg, Afrika Kusini.
Kadhalika alilimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwam-ba ndiye alisaidia kuhara-kishwa kwa mchakato wa kuhamishiwa jijini hapa kwa ajili ya matibabu zaidi ambayo yamemrejeshea uzima ambao tayari ulikuwa kama umepotea. “
Kwa kweli sasa kama mnavyoniona sijambo sana. Nimeanza kufanya mazoezi. Sijambo kwa kweli inga-wa bado niko hospitalini naendelea na matibabu,” alisema Manumba.
Wakati huohuo, Mwe-nyekiti wa Jukwaa la Waha-riri Tanzania (TEF), Absa-lom Kibanda, amezungum-zia tukio la kuvamiwa kwake huku akiweka bayana kuwa, watesi wake walikusudia kumtoa uhai.
“Kwa muda mrefu nili-kuwa nimedokezwa na rafiki yangu mmoja kuwa ninapokwenda nyumbani niwe mwangalifu kuanga-lia nani hasa yuko nyuma yangu usiku, lakini kwa siku ile sikuona kama kuna watu walikuwa wakinifuatilia,” alisema katika mahojiano na gazeti Mwananchi.

Alisema anachokiamini ni kwamba shambulizi dhidi yake linatokana na kazi yake ya uandishi wa habari ija-pokuwa hafahamu ni kazi ipi ambayo inaweza kuwa kichocheo cha kujeruhiwa kwake.

Source: Mwananchi

No comments: