Thursday, July 11, 2013

Kikwete awaka CHADEMA kuanzisha kikosi cha ulinzi


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ameionya kuhusu uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi ndani ya  vyama vya siasa na kusema ni kinyume cha sheria.

Akizungumza katika Kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia, Tanzania Center for Democracy TCD, Rais amesema vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili ya kulinda raia na mali zao , hivyo kuanzisha vyombo vingine nje ya vyombo hivyo vilivyopewa majukumu hayo ni kuvunja sheria.

Kauli ya Rais Kikwete inakuja siku moja baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kuwa kimeamua kuanzisha vikosi vya ulinzi ndani ya chama vitakavyokuwa na majukum ya kulinda viongozi wa chama hicho.