Monday, July 18, 2011

Bajeti ya Ngeleja ya Nishati na madini yakwama

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja

Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo William Ngeleja hii imekwama bungeni baada ya wabunge kutoka pande zote, ule wa chama tawala na upinzani kuipinga kwa maelezo kwamba haina mipango ya kuondoa tatizo la sasa la mgao wa umeme.

Ilibidi  Waziri Ngeleja amwachie Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda ambaye imelieleza Bunge kuwa serikali inaomba muda wa wiki tatu ili kuifanyia marekebisho bajeti hiyo.

Tangu ijumaa wiki iliyopita Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na Waziri Ngeleja ilikuwa ikipingwa vikali na wabunge hasa kuhusu  mikataba ya madini na tatizo la mgao wa umeme.

Bajeti hiyo inatarajiwa kusomwa upya Agosti 13, mwaka huu.

No comments: