Monday, October 3, 2011

CHADEMA yaitoa jasho CCM Igunga

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeonyesha uwezo mkubwa wa kukikabili chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapunduzi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zinasubiri kuthibitishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Igunga, Chama cha Mapinduzi kinaongoza kwa kiasi kidogo katika kura ambazo zimeshahesabiwa hadi hivi sasa.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari ndani ya ukumbi wa kujumlishia kura mgombea wa CCM Dr. Dalali Kafumu amepata kura 25,000 wakati mgombea wa CHADEMA Joseph Kashindye namkaribia kwa karibu ambapo amepata kura 21,000.

Hadi sasa kura bado zinaendelea kujumlishwa ili kila mmoja ajulikane amepata kura ngapi

No comments: